GABON 2017 |
GUINEA- BISSAU |
MASHINDANO
ya 31 ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2017, yataanza leo Jumamosi
Januari 14 huko Gabon kwa Wenyeji hao kuivaa washiriki wa mara ya kwanza
kabisa Guinea-Bissau katika Mechi ya Kundi A.
Nchi
16 zilizogawanywa Makundi Manne ya Timu 4 kila moja zitashiriki
michuano hii ambayo Fainali yake itakuwa Februari 5 na kuchezwa kwenye
Viwanja Vinne vya Miji ya Libreville, Franceville, Oyem na Port Gentil
huko Gabon.
Mashindano
haya, ambayo yalichezwa kwa mara ya kwanza Nchini Sudan Mwaka 1957 na
kushirikisha Nchi 3 tu na Egypt kutwaa Ubingwa, yatakuwa Na Mechi 32
ndani ya Siku 23 huyu Mshindi, atakaepatikana kwenye Fainali Februari 5,
akizoa kitita cha Dola Milioni 4.
WENYEJI.
Hii
itakuwa mara ya pili kwa Gabon kuwa Wenyeji wa AFCON kwani Miaka Mitano
iliyopita wao na Equatorial Guinea ndio walikuwa Wenyeji na safari hii
kufanikiwa tena Uenyeji baada ya CAF kuiondoa Libya, iliyopaswa kuwa
Wenyeji 2013, kutokana na Vita na Mwaka huo kuchezwa Afrika Kusini
waliotakiwa kuwa Wenyeji wa Mwaka 2017.
Gabon,
Nchi ya Watu Milioni 1 Laki 8, ipo Nafasi ya 108 katika Listi ya FIFA
ya Ubora Duniani ingawa wanae mmoja wa Mastraika hatari Duniani
Pierre-Emerick Aubamenyang anaecheza Bundesliga huko Germany katika Klabu ya
Borussia Dortmund.
WACHEZAJI AMBAO WATAVUTIA KATIKA FAINALI HIZI.
AUBAMEYANG. |
Mbali
ya Aubameyang, macho ya wengi yatawafuatilia Mchezaji Bora Afrika Riyad
Mahrez wa Mabingwa wa England Leicester City anaechezea Algeria na
Sadio Mane wa Liverpool anaecheza Senegal.
RIYAD MAHREZ. |
Pia
wapo Wachezaji wengine 23 wanaocheza EPL, Ligi Kuu England, na hao ni
pamoja na Sentahafu wa Manchester United Eric Bailly wa Mabingwa
Watetezi Ivory Coast, Fowadi wa West Ham wa Ghana Andre Ayew, wa
Leicester Islam Slimani anaecheza Algeria na Winga wa Crystal Palace
atakaecheza Ivory Coast Wilfried Zaha.
Zaha
ameamua kuichezea Ivory Coast hivi Juzi tu baada ya kuwahi kuzichezea
Timu za Vijana za England na Majuzi kufunga Bao lake la kwanza kwa Nchi
yake walipopasha na Uganda.
Wachezaji wengine mvuto ni yule wa Egypt Mohamed Salah anaecheza Serie A na AS Roma baada kuhama kutoka Chelsea. Lakini
Historia itamgusa Kipa wa Egypt Essam El Hadary ambae anaweza kuweka
Rekodi ya kuwa Mchezaji mwenye Umri kubwa kabisa kuwahi kucheza Fainali
za AFCON ikiwa atacheza kwani atatimiza Mika 44 hapo Januari 15.
Egypt ndio Nchi inayomeremeta Afrika kwa kutwaa Ubingwa mara nyingi, mara 7.
KOCHA WA KIHISTORIA
Mfaransa
Herve Renard anawania kuwa Kocha wa kwanza kutwaa Ubingwa wa Afrika
mara 3 na Nchi 3 tofauti baada ya kuiongoza Zambia Mwaka 2012 na Ivory
Coast katika Mashindano yaliyopita na safari hii yupo na Morocco.
Makocha
wengine waliowahi kutwaa Ubingwa wa Afrika mara 3 ni Charles Gyamfi
akiwa na Ghana Miaka ya 1963, 1965 na 1982 na Hassan Shehata akiwa na
Egypt Miaka ya 2006 na 2010.
VIWANJA VITAKAVYOTUMIKA.
Viwanja
vitakavyotumika ni Stade de l’AmitiĆ© huko Libreville, Gabon, unaochukua
Watu 38,000, ambako Kundi A ndio litacheza Mechi zake, na kingine cha
Kundi B ni Port Gentil Stadium, Port Gentil, wenye kuchukua Washabiki
20,000, Kundi C lipo Stade de Franceville Mjini Franceville wenye uwezo
wa Watu 20,000 wakati Kundi D litakuwa huko Oyem Stadium ulioko Assok
Ngomo, Gabon, uwezo 20,000.
Mabingwa
Watetezi wa Afrika ni Ivory Coast lakini safari hii watawakosa
Wachezaji wao wakubwa, wale Ndugu Toure, yaani Yaya na Kolo, ambao
wamestaafu, na Majeruhi ambae ni Gervinho.
MABINGWA WATETEZI
Ivory Coast walitwaa Ubingwa wa Afrika huko Equatorial Guinea Mwaka 2015.
Wenyeji Gabon wapo Kundi A pamoja na Burkina Faso, Cameroon na Guinea-Bissau iliyotinga Fainali kwa mara ya kwanza.
JIRANI YETU
Jirani
zetu Uganda wapo kundi D pamoja na Ghana, Mali na Egypt ambao wanarejea
kwenye Fainali hizi kwa mara ya kwanza tangu watwae Ubingwa Mwaka 2010.
0 Maoni:
Post a Comment