Zlatan
Ibrahimovic ametwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa EPL, Ligi Kuu England, kwa
Mwezi Desemba na mwenzake wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan kuzoa
ile ya Goli Bora.
Ibrahimovic,
Mchezaji kutoka Sweden mwenye Miaka 35, alifunga Bao 5 Mwezi Desemba na
sasa ana Jumla ya Mabao 18 tangu ajiunge na Man United mwanzoni mwa
Msimu.
Desemba
alifungua akaunti yake kwa Bao dhidi ya Everton huko Goodison Park na
kisha kupiga Bao la ushindi kule Selhurst Park walipoicharanga Crystal
Palace 2-1.
The
Hawthorns ilishuhudia Ibrahimovic akipiga 2 wakati Man United inaipiga
West Bromwich Albion 2-0 na kuifunga Sunderland 1 Siku ya Boksing Dei.
Pia, Ibrahimovic alifunga wakati Man United inaibwaga Zorya Luhansk 2-0 kwenye UEFA EUROPA LIGI huko Ukraine.
Tuzo
hii kwa Ibrahimovic inafuatia zile za Raheem Sterling wa Manchester
City, Son Heung-min wa Tottenham Hotspur na Wawili wa Chelsea Eden
Hazard na Diego Costa kwa Msimu huu.
Tuzo
nyingine ya Goli Bora la Mwezi imekwenda kwa Mchezaji mwingine wa
Manchester United, Henrikh Mkhitaryan, kwa Bao lake la ushindi dhidi ya
Sunderland ambalo limebatizwa ‘Kiki ya Nge’, Scorpion Kick.
0 Maoni:
Post a Comment