DROO
ya Robo Fainali ya Copa del Rey, Kombe la Mfalme huko Spain, imefanyika
na Mabingwa Watetezi FC Barcelona watacheza na Real Sociedad wakati
Celta Vigo wakipangwa na Mahasimu wao wakubwa Real Madrid.
Juzi Real walitinga Robo Fainali baada ya kusawazisha Dakika za Majeruhi na kupata Sare ya 3-3 walipocheza Ugenini na Sevilla na kuweka Rekodi ya kutofungwa katika Mechi 40 mfulululizo.
Real walishinda Mechi ya Kwanza 3-0.
Barca wao waliwatoa Athletic Bilbao kwa Jumla ya Bao 4-3 baada ya kufungwa Mechi ya Kwanza 2-1 na wao Juzi kushinda 3-1 Nou Camp.
Mechi nyingine za Robo Fainali ni Atletico Madrid kucheza na Eibar wakati Alcorcon, Timu pekee ambayo haipo La Liga na ipo Daraja la Chini, itacheza na Alaves.
Mechi hizi za Robo Fainali zitachezwa kwa Mikondo Miwili ya Nyumbani na Ugenini hapo Januari 18 na Marudiano Wiki Moja baadae.
Fainali ya Copa del Rey itafanyika Mei 27.
0 Maoni:
Post a Comment