MASHINDANO
ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2017, yataanza Jumamosi Januari 14
huko Gabon na kushirikisha Nchi 16 zilizogawanywa Makundi Manne ya Timu
4 kila moja.
AFCON,
ambayo Fainali yake itakuwa Februari 5, itachezwa kwenye Viwanja Vinne
vya Miji ya Libreville, Franceville, Oyem na Port Gentil.
Viwanja
vitakavyotumika ni Stade de l’Amitié
Stade de l’Amitié |
huko Libreville, Gabon, unaochukua
Watu 38,000, ambako Kundi A ndio litacheza Mechi zake, na kingine cha
Kundi B ni Port Gentil Stadium, Port Gentil,
Port Gentil Stadium, |
wenye kuchukua Washabiki
20,000, Kundi C lipo Stade de Franceville Mjini Franceville
Stade de Franceville |
wenye uwezo
wa Watu 20,000 wakati Kundi D litakuwa huko Oyem Stadium ulioko Assok
Ngomo,
Gabon, uwezo 20,000.
Oyem Stadium |
Mabingwa
Watetezi wa Afrika ni Ivory Coast lakini safari hii watawakosa
Wachezaji wao wakubwa, wale Ndugu Toure, yaani Yaya na Kolo, ambao
wamestaafu, na Majeruhi Yao Gervinho.
**********************************************
MAKUNDI:
KUNDI A: Gabon, Burkina Faso, Cameroon, Guinea-Bissau
KUNDI B: Algeria, Tunisia, Senegal, Zimbabwe
KUNDI C: Ivory Coast, DR Congo, Morocco, Togo
KUNDI D: Ghana, Mali, Egypt, Uganda
************************************************
Ivory Coast walitwaa Ubingwa wa Afrika huko Equatorial Guinea Mwaka 2015.
Wenyeji Gabon wapo Kundi A pamoja na Burkina Faso, Cameroon na Guinea-Bissau iliyotinga Fainali kwa mara ya kwanza.
Jirani
zetu Uganda wapo kundi D pamoja na Ghana, Mali na Egypt ambao wanarejea
kwenye Fainali hizi kwa mara ya kwanza tangu watwae Ubingwa Mwaka 2010.
0 Maoni:
Post a Comment