Kocha
wa zamani wa Simba, Mcroatia, Zdravko Logarusic, amesaini mkataba wa
miaka miwili ya kuinoa timu ya Asante Kotoko ya Ghana baada ya kuachana
na Interclube ya Angola.
Logarusic
ambaye aliinoa Simba kuanzia Desemba, 2013 mpaka Julai, 2014, Novemba
mwaka jana alimaliza mkataba wa kuifundisha Interclube huku akifanikiwa
kuipa kombe la chama cha soka la nchi hiyo, APFL.
Mtandao wa habari za michezo wa Ghana unaojulikana kama Ghana Soccernet, jana Jumanne uliripoti kuwa:
“Asante
Kotoko imeingia mkataba wa miaka miwili na kocha raia wa Croatia,
Zdravko Lugarusic, ataanza kuinoa timu hiyo ndani ya wiki hii baada ya
kukamilisha taratibu za kupata kibali cha kazi.”
Ikumbukwe
kuwa, Asante Kotoko ilikuwa haina kocha mkuu tangu Machi, mwaka jana
baada ya aliyekuwa kocha wao, David Duncan kuachia ngazi kutokana na
matokeo mabaya aliyokuwa akiyapata. Kwa muda wote huo, kikosi hicho
kilikuwa chini ya kocha msaidizi, Michael Osei.
0 Maoni:
Post a Comment