ARSENAL YAANZA MWAKA KWA USHINDI DHIDI YA BIG SAM

Tokeo la picha la ARSENAL IMAGE VS CRYSTAL PALACE
Arsenal wameanza vyema Mwaka Mpya 2017 kwa kuichapa Crystal Palace 2-0 huko Emirates na kukamata Nafasi ya Tatu kwenye EPL, Ligi Kuu England.
 
EPL, ambayo sasa imeshachezwa Mechi 19 kati ya 38 za Msimu mzima, inaongozwa na Chelsea wenye Pointi 49 wakifuatiwa na Liverpool wenye 43, kisha Arsenal wenye 40 na kufuatiwa Tottenham na Man City zenye 39 kila mmoja huku ya 6 ikiwa Man United yenye Pointi 36.
Bao la kwanza la Arsenal lilifungwa na Olivier Giroud kwa Kisigino katika Dakika ya 17 na kudumu hadi Mapumziko.
 Tokeo la picha la GIROUD IMAGE SCORPION KICK

Arsenal wakapiga Bao la Pili Dakika ya 56 kupitia Alex Iwobi.
Katika Mechi ya kwanza ya EPL iliyochezwa hii Leo, Harry Kane na Dele Alli alipiga Bao 2 kila Mtu wakati Tottenham ikiwatwanga Watford waliodorora 4-1 na kutinga kwenye 4 Bora ya EPL kwamara ya kwanza tangu Oktoba.
EPL itaendelea tena Jumatatu kwa Mechi 6.

VIKOSI:
Arsenal: Cech; Bellerín, Gabriel, Koscielny, Monreal; Elneny, Xhaka; Lucas Pérez, Iwobi, Sánchez; Giroud.
Akiba: Ospina, Ramsey, Oxlade-Chamberlain, Mustafi, Reine-Adélaïde, Coquelin, Maitland-Niles.

Crystal Palace: Hennessey; Ward, Dann, Tomkins, Kelly; Flamini, Puncheon, Cabaye; Townsend, Zaha, C Benteke.
Akiba: Speroni, Campbell, Lee, Fryers, Mutch, Sako, Husin.
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment