SIMBA YAANZA MAPINDUZI CUP KWA USHINDI

 Tokeo la picha la simba image mapinduzi cup
MASHINDANO ya Kombe la Mapinduzi ya kuenzi Miaka 53 tangu Mapinduzi tukufu ya Visiwa vya Zanzibar na Pemba, ambayo yalianza kwa Mechi moja ya Kundi A, yameendelea huko Amaan Stadium, Zanzibar kwa Mechi nyingine mbili za Kundi A.
 
Katika Mechi ya kwanza Juzi Usiku, Timu pinzani huko Zanzibar zilipambana na Taifa Jang’ombe kuifunga Jang’ombe Boys 1-0.

Katika Mechi ya kwanza ya hii Leo iliyochezwa mapema, KVZ ya Zanzibar ilichapwa 2-0 na URA ya Uganda, ambao ndio Mabingwa Watetezi, na Usiku, Vinara wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, Simba, walitinga Amaan Stadium kwa kucheza na Taifa Jang’ombe.

Katika Mechi hiyo, Simba walipata Bao la Kwanza Dakika ya 27 ambalo Muzamil Yasin alifunga na kupiga la Pili Dakika ya 41 Mfungaji akiwa Juma Luizio.

Dakika ya 76, Lufungo wa Simba alijifunga mwenyewe na kuipa Taifa Jang’ombe Bao na kufanya Gemu iwe 2-1.
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment