Ligi Kuu England Ratiba
!!!Saa za Bongo!!!
Jumatatu Januari 2
1530 Middlesbrough v Leicester City
1800 Everton v Southampton
1800 Manchester City v Burnley
1800 Sunderland v Liverpool
1800 West Bromwich Albion v Hull City
2015 West Ham United v Manchester United
***************************************
LEO Vigogo wa Soka wa EPL, Ligi Kuu England, Manchester
United wanatua huko London Stadium Jijini London kucheza na Timu ngumu
West Ham katika Mechi ya Ligi hiyo wakiwa kwenye wimbi tamu la ushindi
wa Mechi 5 mfululizo na kutofungwa katika Mechi zao 12 zilizopita.
Leo,
Jose Mourinho, Meneja wa Man United, anataka kuuanza Mwaka Mpya 2017
kwa mguu mzuri kwa kusaka ushindi dhidi ya West Ham ambayo Msimu
uliopita kwenye Mechi kama hii ya EPL kwenye Uwanja wao wa zamani Upton
Park walishinda 3-2.
Lakini
Msimu huu, Timu hizi zimeshakumbana mara 2 na Man United kutoka 1-1 na
West Ham, chini ya Meneja Slaven Bilic, kwenye EPL na Siku 4 baadae
kupambana kwenye Robo Fainali ya EFL CUP na Man United kuibuka kidedea
kwa Bao 4-1.
Kwenye
Mechi hii, Man United itamkosa Beki wao mahiri Eric Bailly ambae Jana
aliondoka Kikosini kwenda kujiunga na Timu ya Taifa ya Ivory Coast kwa
ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2017.
Wengine
wa Man United ambao hawatakuwepo ni Majeruhi Luke Shaw na wenye
hatihati kucheza ni Kepteni Wayne Rooney mwenye maumivu ya Paja na
Michael Carrick ambae alikuwa Mgonjwa.
Kwa
upande wa West Ham, wana Wachezaji kadhaa ambao ni Majeruhi na hao ni
Diafra Sakho, Arthur Masuaku, Alvaro Arbeloa na Gokhan Tore huku wenye
hatihati ni Nahodha wao Mark Noble alieumizwa Juzi kwenye Mechi yao na
Leicester na kulazimika kubadilishwa na pia wengine wenye hatihati ni
Daniel Amartey, Byram na Zaza.
Licha
ya upungufu huo, West Ham wameibuka upya hasa baada ya kurejea Kikosini
mwao kwa Majeruhi Andy Carroll na Andre Ayew lakini Man United ya sasa,
iliyofufuka upya baada ya kucharazwa na Chelsea Mwezi Oktoba si mchezo.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
WEST HAM: Randolph, Nordtveit, Reid, Ogbonna, Cresswell, Lanzini, Kouyate, Antonio, Ayew, Payet, Carroll
Akiba kutokana na: Adrián, Spiegel, Feghouli, Zaza, Byram, Fletcher, Calleri, Noble
MAN UNITED: De Gea, Valencia, Jones, Rojo, Darmian, Fellaini, Herrera, Pogba, Rashford, Ibrahimovic, Martial
Akiba kutokana na:
Romero, Johnstone, Depay, Fosu-Mensah, Tuanzebe, Schneiderlin, Young,
Blind, Schweinsteiger, Lingard, Smalling, Mkhitaryan, Mata, Rooney,
Carrick
REFA: Mike Dean
EPL – Ligi Kuu England
Jumanne Januari 3
2245 Bournemouth v Arsenal
2300 Crystal Palace v Swansea City
2300 Stoke City v Watford
Jumatano Januari 4
2300 Tottenham Hotspur v Chelsea
0 Maoni:
Post a Comment