SCORPION KICK ZA FUNGA MWAKA NA FUNGUA MWAKA HIZI HAPA

 Tokeo la picha la GIROUD IMAGE SCORPION KICK
Siku sita zilizopita, kiungo Henrikh Mkhitaryan wa Man United alifunga bao safi wakati timu yake ikivaa Sunderland.
Bao hilo lilikuwa gumzo na kupewa jina la Scorpion Kick. Lakini siku sita baadaye unaweza kusema amepata jibu.
ANGALIA VIDEO YA SCORPION KICK YA GIROUD HAPA.

Olvier Giroud wa Arsenal naye amefunga bao linalofanana na hilo katika mechi dhidi ya Crystal Palace ambayo Arsenal imeibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Sasa ni gumzo, kwamba bao hilo la Mhkitaryan raia wa Armenia na lile la Giroud kutoka Ufaransa. Lipi kali hasa?
 

Kila mmoja anaweza kuwa huru kupitia maoni yake pamoja na ushabiki. Lakini ukweli ni hivi; bao la Mkhitaryan lilikuwa bora la funga mwaka 2016 na lile la Giroud limekuwa bora la fungua mwaka 2017.
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment