Real Madrid wameikamata Rekodi ya Barcelona ya kutofungwa katika
Mechi 39 za Mashindano yote baada ya kuitandika Granada 5-0 katika
Mechi yao ya kwanza ya Mwaka 2017 ya La Liga iliyochezwa Santiago
Bernabeu Jijini Madrid Nchini Spain.
Ushindi huo umeifanya Real izidi kuongoza La Liga sasa ikiwa Pointi
6 mbele ya Timu ya Pili FC Barcelona ambao ndio Mabingwa Watetezi.
Bao za Real zilipachikwa wavuni na Isco, Dakika za 12 na 31, Karim Benzema, 20, Cristiano Ronaldo, 27 na Casemiro, 58.
0 Maoni:
Post a Comment