ARSENAL YASHINDA 4, HUKU IKISAIDIWA GOLI 2.

Tokeo la picha la ARSENAL VS SWANSEA IMAGE

Mechi 6 za EPL, Ligi Kuu England, zilizoanza Saa 12 Jioni zimemalizika na Burnley, Hull City, Stoke City, Arsenal na West Ham kutoka na ushindi wakati Watford na Middlesbrough zikitoka 0-0.
 
Burnley iliichapa Southampton 1-0 kwa Bao la Dakika ya 77 la Joey Barton aliefunga kwa Frikiki katika Mechi yake ya kwanza tangu ahamie hapo.

Nao Hull City wameichapa Bournemouth 3-1 kwa Bao 2 za Hernandes na moja la Mings aliejifunga mwenyewe wakati lile la Bournemouth likifungwa na Stanislas kwa Penati ya Dakika ya 3 tu.

Sunderland, wakiwa kwao Stadium of Light, walinyukwa 3-1 na Stoke City waliopata Bao zao kupitia Marko Arnautovic, Bao 2, na Peter Crouch wakati Jermaine Defoe aliipa Sunderland Bao lao pekee. 

Arsenal, wakicheza Ugenini, waliichara Swansea City 4-0 kwa Bao za Olivier Giroud, Alexis Sanchez na 2 walizojifunga wenyewe Swansea kupitia Cork na Naughton.

West Ham wameitandika Crystal Palace 3-0 kwa Bao za Sofiane Feghouli, Manuel Lanzini na Andy Carroll.

 EPL-JAN14A
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment