Kocha Mkuu wa Arsenal, Arsene Wenger ameongoza zoezi la kuwabakiza klabuni hao wachezaji watatu muhimu.
Wenger ameongoza zoezi la kuwaongeza mkataba mshambuliaji Olivier Giroud na walinzi Laurent Koscielny na Francis Coquelin.
Taarifa
zinasema baada ya hao wawili, Arsenal itakuwa na kazi nyingine ya
kuhakikisha inawaongezea mkataba vigogo Mesut Ozil na Alexis Sanchez.
Koscielny
mwenye umri wa miaka 31, amesaini mkataba mpya hadi mwaka 2020, Giroud
mkataba wake utaisha 2019 yaani mwaka keshokutwa na Coquelin amesaini
mkataba wa miaka minne na nusu.
0 Maoni:
Post a Comment