BAO
la BENZEMA la dakika ya 90 na ushei limesaidia Real Madrid kupata
suluhu ya 3-3 walipocheza Ugenini na Sevilla katika Mechi ya Pili ya
Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Copa del Rey na kutinga Robo Fainali kwa
Jumla ya Bao 6-3 kwa Mechi 2 lakini pia kuweka Rekodi huko Spain ya
kutofungwa katika Mechi 40.
Wakiwa
wameshinda 3-0 huko kwao Santiago Bernabeu wakicheza bila ya Masta wao
kadhaa akiwemo pia Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo Usiku huu pia
huko walicheza bila ya hao.
Real
walijikuta wako nyuma 1-0 katika Dakika ya 10 baada ya Danilo kujifunga
na kusawazisha Dakika ya 48 kwa Bao la Marco Asensio lakini wakajikuta
wako 3-1 nyuma kwa Bao za Sevilla zilizofungwa Dakika za 53 na 77 na
Jovetic na Iborra.
Kepteni Sergio Ramos aliipa Real Bao la Pili Dakika ya 83 na Karim Benzema, alieingizwa mwishoni, kusawazisha Dakika ya 93.
0 Maoni:
Post a Comment