IBRAHIMOVIC AIKOMBOA MAN U, YAAMBULIA SARE.

Tokeo la picha la MAN U VS LIVERPOOL IMAGE
MAHASIMU wa Jadi huko England, Manchester United na Liverpool wametoka Sare 1-1 katika Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, iliyochezwa Uwanjani Old Trafford Mjini Manchester.
 
Kwenye Mechi ya Kwanza ya EPL Msimu huu Timu hizi zilitoka 0-0 huko Anfield na Leo Man United waliingia kwenye mtanange huu wakiwa hawajafungwa katika Mechi 15 zilizopita huku wakishinda Mechi 6 za EPL mfululizo wakati Liverpool, baada ya kuichapa Man City 1-0 Desemba 31, hawajashinda hata Mechi baada kufungwa 1 na Sare 2.

Lakini jana Liverpool walianza vyema kwa kufunga Bao la Penati ya Dakika ya 27 iliyopigwa na James Milner ambayo ilitolewa baada ya Kona ya Milner kudaiwa na Refa Michael Oliver ilishikwa kwa makusudi na Paul Pogba wakati Kiungo huyo wa Man United hakuwa akitazama Mpira na wala hakuinua Mkono juu akiwa kwenye harakati za kummaki Mchezaji wa Liverpool Dejan Lovren, kitu ambacho Wachambuzi wengi huko England walikiunga mkono.
 Picha inayohusiana

Licha ya kupata nafasi nyingi za kufunga, Man United walingojea hadi Dakika ya 84 pale Zlatan Ibrahimovic aliposawazisha baada kutokea kizaazaa langoni mwa Liverpool kufuatia Kichwa cha Marouane Fellaini kugonga Posti na kumrejea Ibrahimovic aliefunga.
 Tokeo la picha la ibrahimovic 2017 image

JE WAJUA KUHUSU HII?
  • Zlatan Ibrahimovic amefunga Bao 14 katika Mechi zake za kwanza 20 za EPL akifungana na Lejendari Alan Shearer na Sergio Aguero.

Matokeo haya yamewaweka Liverpool Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 45 sawa na Timu ya Pili Tottenham huku Vinara Chelsea wakiongoza wakiwa na Pointi 52.

Man United wako pale pale Nafasi ya 6 wakiwa na Pointi 40 na Nafasi ya 5 wako Man City wenye 42 na Arsenal ni wa 4 wakiwa na Pointi 44.

Mechi zijazo kwa Timu Man United na Liverpool ni Jumamosi ijayo wakati Liverpool wako kwao Anfield kucheza na Swansea City wakati Man United wako Ugenini kuivaa Stoke City.

VIKOSI:
MANCHESTER UNITED: De Gea, Valencia, Jones, Rojo, Darmian [Fellaini 76'], Carrick [Rooney 45'], Herrera, Mkhitaryan, Pogba, Martial [Mata 65'] Ibrahimovic
Akiba: Romero, Fellaini, Blind, Smalling, Rooney, Mata, Rashford

LIVERPOOL: Mignolet, Alexander-Arnold, Lovren, Klavan, Milner, Henderson, Can, Lallana, Wijnaldum, Firmino, Origi [Coutinho 61']
Akiba: Karius, Gomez, Moreno, Stewart, Ejaria, Coutinho, Sturridge
Tokeo la picha la Michael Oliver image
Michael Oliver
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment