SENEGAL YAANZA AFCON 2017 KWA USHINDI

Tokeo la picha la KIKOSI CHA SENEGAL AFCON 2017 IMAGE

BAADA kuanza kwa Sare katika Mechi 3 za kwanza za Mashindano ya 31 ya Fainaliza Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2017, Senegal imekuwa Nchi ya kwanza kuzoa Pointi 3 baada ya Jana kuifunga Tunisia Bao 2-0 huko Port Gentil Stadium, Mjini Port Gentil, Nchini Gabon kwenye Mechi ya Kundi B.
 
Juzi, Fainali hizi zilianza kwa Mechi za Kundi A na zote kwenda Sare. Senegal walitangulia kufunga kwa Penati ya Dakika ya 10 iliyopigwa na Mchezaji anaechezea Klabu ya Liverpool, Sadio Mane, na kisha kuongeza Bao la Pili Dakika ya 30 Mfungaji akiwa Kara Mbodji.

Katika Mechi nyingine ya Kundi B iliyochezwa mapema huko huko Port Gentil Stadium, Algeria walijinusuru baada ya Mchezaji Bora wa Afrika, Riyad Mahrez, kuwafungia Bao 2 na kutoka Sare ya 2-2 na Zimbabwe.

Algeria walitangulia kufunga Dakika ya 12 kwa Bao la Dakika ya 12 la Mahrez lakini Zimbabwe wakajibu Dakika za 16 na 29 kupitia Kudakwashe Mahachi na Penati ya Nyasha Mushekwi.Tokeo la picha la MAHREZ IMAGE AFCON 2017

Hata hivyo, Algeria walipata Sare Dakika ya 82 kwa Bao jingine la Mahrez.

Matokeo ya Mechi hizo mbili za Kundi B yamewafanya Senegal, ambao hawajawahi kutwaa Ubingwa wa Afrika ila walifika Fainali ya Mwaka 2002 na kutolewa kwa Penati na Cameroun, wawe kileleni.

Leo zipo Mechi 2 za Kundi C kwa Mabingwa Watetezi Ivory Coast kuanza na Togo
Na kisha Congo DR kucheza na Morocco.
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment