SEVILLA YAZIMA REKODI YA MADRID KWA GOLI LA DAKIKA YA 91

Tokeo la picha la SEVILLA VS MADRID IMAGE 2017
VINARA wa La Liga Real Madrid Jana walichapwa 2-1 Ugenini na kuvunjwa mbio zao za kutofungwa kwa Mechi 40 baada ya Bao la Dakika za Majeruhi la Stevan Jovetic kuwapa Sevilla ushindi wa 2-1.
 
Real ndio waliotangulia kufunga Dakika ya 67 kwa Penati ya Cristiano Ronaldo iliyotolewa baada ya Dani Carvajal kuangushwa na Kipa wa Sevilla Sergio Rico.

Dakika ya 85, Sevilla walisawazisha kwa Bao la kujifunga mwenyewe Sergio Ramos na Dakika ya 91 Jovetic kuwapa ushindi Sevilla.
Tokeo la picha la SEVILLA VS MADRID IMAGE 2017

Matokeo haya bado yamewabakisha Real, ambao walikuwa hawajafungwa tangu Aprili 6, kileleni mwa La Liga wakiwa Pointi 1 mbele ya Sevilla huku Barcelona wakifuatia wakiwa Pointi 2 nyuma yao lakini Real wamecheza Mechi 1 pungufu kupita Wapinzani wao wote.

Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment