MOURINHO NA PENATI YA POGBA ASEMA; MECHI TATU, PENATI 3 HUKU MAN U AKIAMBULIA SARE.

Tokeo la picha la MOURINHO IMAGE

PENATI waliyopewa Liverpool hapo Jana huko Old Trafford na kuzaa Bao lao katika Sare ya 1-1 na Manchester United imezua mjadala na mabishano makubwa kila kona ya Soka.
 
Penati hiyo ilitolewa Dakika ya 26 na Refa Michael Oliver kwa madai Paul Pogba alinawa kwa makusudi Kona ya James Milner.
 Tokeo la picha la MILNER PENATI IMAGE 2017
Baada ya Mechi hiyo, Wanahabari walimwandama Meneja wa Man United Jose Mourinho atoboe ya moyoni kuhusu kutolewa kwa Penati hiyo.
 
Na Mourinho, ambae Msimu huu amekuwa matatani mara 2 na FA, Chama cha Soka England, kuhusu kauli zake juu ya Marefa na kushushiwa Faini na Kifungo, alikuwa mwangalifu mno kuhusu majibu yake.
 
Mourinho aliwajibu: "Sijui. Sijui. Sikuona lakini Refa alikuwa karibu pengine ni Penati. Tatizo la Penati si mazingira tu, wakati mwingine inatolewa, mara nyingine hapana. Inashangaza hizi ni Mechi 19, 21, 21 za Ligi Kuu, pia 3 za Kombe la Ligi na moja ya FA CUP, jumla Mechi 25, na katika Mechi 25 tumepewa Penati 1 tu. 
 
Lakini leo ilikuwa kwenye Boksi letu. Sikuiona lakini inabidi niamini ni Penati. Nimefurahi kuhusu Refa kama ni Penati kwa rekodi yake kwetu Mechi 3 Penati 3 dhidi yetu!"
 
Msimu huu, Refa Michael Oliver ametoa Penati 3 dhidi ya Man United kwenye Mechi zao na Watford, Everton na hiyo na Liverpool.
 Picha inayohusiana
Penati pekee waliyopewa Man United ni kwenye Mechi yao ya Ligi Msimu huu dhidi ya Southampton.
Pia, kwenye UEFA EUROPA LIGI, wakiitwanga Feyenoord walishinda Penati 2.
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment