KUELEKEA AFCON GABON 2017, IJUE MIPIRA ILIYOWAHI KUTUMIKA KATIKA FAINALI ZILIZOPITA.


Kuelekea mashindano makubwa ya Afcon 2017 yatakayoanza KESHO jumamosi kiungomshambuliaji.blogspot.com inakueletea list ya mipira iliyowahi kutumika katika mashindano yaliyopita.

Huku tukisubiri kuona ni mpira gani utatumika mwaka huu kutoka kwa watengenezaji Adidas.

MPIRA AINA YA WAWA ABA- AFCON 2008

Aina hii ya mpira ilitumika mwaka 2008 katika fainali za nchini Ghana.

Jina hili ni asili ya Afrika Magharibi.
 

MPIRA AINA YA JABULANI ANGOLA

Jabulani Angola ni mpira uliotumika  katika fainali za mwaka 2010 zilizofanyika nchini Angola. 
Lakini Aina hii ya mpira ya Jabulani ulitumika pia katika kombe la Dunia mwaka 2010.


MPIRA AINA YA COMOEQUA

Katika fainali za mwaka 2012 mpira ulopewa jina la Comoequa uliweza kutumika katika fainali za mwaka huo nchini Gabon na Equatoril Guinea.

Aina hii ya mpira inafanana na namna mpira wa Tango ulivo kutokana na kutengenezwa kwa mfano wa Tango.


 MPIRA AINA YA KATLEGO

Katika fainali za mwaka 2013 aina ya mpira wa Katlego ulipitishwa kutumika katika fainali za nchini Afrika Kusini.

MPIRA AINA YA MARHABA NDANI YA AFCON

Jina ambalo lina asili ya Uarabu yaani Marhaba lilikua jina la mpira uliotumika katika fainali za mwaka 2015 katika nchi ya E. Guinea.

Ambapo mshindi wa Fainali hizo alikiwa Ivory Coast.
 

Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment