Simba huenda wakamkosa kiungo wa mshambuliaji Mohamed Ibrahim katika mechi ya fainali Kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam FC leo.
Simba itashuka dimbani Amaan kuivaa Azam FC katika mechi ya Kombe la
Mapinduzi. Azam ikiwa na rekodi ya kutofungwa hata goli moja katika
michuano hiyo msimu huu.
Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amesema bado hali ya Mo Ibrahim haijaimalika kwa asilimia mia.
“Kila kitu kinakwenda vizuri na maandalizi ni mazuri. Lakini Ibrahim,
hali yake bado si asilimia mia. Hivyo ni suala la kuendelea kuangalia,”
alisema.
Mo Ibrahim alilazimika kutoka nje na nafasi yake kuchukuliwa na
Laudit Mavugo katika mechi ya nusu fainali dhidi Yanga. Simba ilishinda
mechi hiyo kwa mikwaju ya penalti 4-2.
Mayanja alisema Simba inatambua mechi hiyo ni ngumu na itapambana vilivyo kuhakikisha inafanikiwa kubeba ubingwa.
Aidha kwa upande wa wapinzani wao, Kocha wa muda wa Azam FC Iddi
Cheche amesema dawa ya Simba katika mechi ya fainali ya Kombe la
Mapinduzi iko tayari, bado kunyweshwa tu.
Simba itashuka dimbani Amaan kuivaa Azam FC katika mechi ya Kombe la
Mapinduzi. Cheche amesema maandalizi yanakwenda vizuri na Simba, haiwezi
kumpa hofu.
"Imebaki kuwanywesha tu dawa yao, nimecheza na Simba wakati nikiwa
mchezaji. Najua aina yao ya uchezaji, kawaida huwa haibadiliki sana.
"Naweza kusema dawa yao imekamilika na kila kitu kitakwenda vizuri," alisema.
Azam FC ambayo ilianza michuano hiyo kwa kusuasua, iliitwanga Yanga
kwa mabao 4-0 katika mechi ya mwisho ya makundi na kutinga nusu fainali
kwa kishindo.
Hali hiyo inaonyesha kuamsha hali ya kujiamini kwa Azam FC ambayo siku chache uongozi wake uliwatimua makocha kutoka Hispania.
0 Maoni:
Post a Comment