AFCON 2017: CAMEROON YATINGA FAINALI.

WACHEZAJI WA CAMEROON WAKISHANGILIA GOLI LAO LA KWANZA.
CAMEROON wameingia Fainali ya AFCON 2017, Kombe la Mataifa ya Afrika, baada kuifunga Ghana 2-0 huko Nchini Gabon.
 
Mechi hii, Ghana walionekana wako juu kidogo lakini kukosa kwao umakini kwa nafasi chache walizopata ndio hasa kumesababisha wapigwe.

Frikiki ya Dakika ya 71 ilizaa Bao kwa Cameroon pale Difensi ya Ghana ilipojichanganya na kumruhusu Ngadeu kufunga. 

Ndani ya Dakika za Nyongeza, kaunta ataki ya Cameroon ilizaa Bao lao la pili kwa Bassogog kuchanja mbuga na Mpira na kumchambua Kipa Brimah na kuipa Cameroon ushindi wa 2-0.

Sasa Cameroon watacheza Fainali na Egypt hapo Jumapili kupata Bingwa wa Afrika wakati Ghana wakicheza Jumamosi na Burkina Faso kusaka Mshindi wa Tatu. 

VIKOSI:
CAMEROON: Ondoa, Oyongo, Fai, Ngadeu, Teikeu, Siani, Djoum, Zoua, Moukandjo, Bassogog, Tambe
GHANA: Brimah; Acheampong, Afful, Amartey, Boye; Wakaso, Acquah, Partey, Atsu, Andre Ayew, Jordan Ayew

AFCON 2017
Ratiba:
**Saa za Bongo**

Mshindi wa 3
Jumamosi Februari 4
2200 Burkina Faso v Ghana

Fainali AFCON 2017
Jumapili Februari 5
2200 Egypt v Cameroon
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment