LA LIGA: REAL WAWAFATA TENA WABABE WAO CELTA VIGO, JE ITALIPA KISASI?

Tokeo la picha la REAL MADRID IMAGE

VINARA wa La Liga Real Madrid Wikiendi hii watacheza Ugenini na Celta Vigo ambayo Wiki mbili zilizopita iliitupa nje Real kwenye Robo Fainali ya Copa del Rey.
 
Kwenye Mechi 2 za Robo Fainali hiyo, Real ilichapwa 2-1 kwao Santiago Bernabeu na kisha kutoka 2-2 Nyumbani kwa Celta Vigo.
 
Mechi hii ni muhimu kwa Real kuzikimbia Barcelona na Sevilla ambazo zinaikimbiza kileleni mwa La Liga.
 
Real, waliocheza Mechi 19, wapo Pointi 4 mbele ya Barca na Sevilla zilizofungana kwa Pointi na zote zikiwa zimecheza Mechi 20.
 
Wikiendi hii Barca wapo kwao Nou Camp kucheza na Athletic Bilbao wakati Sevilla pia wapo Nyumbani kucheza na Villareal.
 
Kwenye Mechi yao hii, Real wanategemewa kuimarika kwa Majeruhi wao kadhaa kurejea na hao ni Pepe, James Rodriguez na Luka Modric.
 
Uimara huo unahitajika kwani Celta Vigo wameshaonyesha ugumu wao kwa Real licha ya kuwa Nafasi ya 8 kwenye La Liga kwani kwa Misimu Miwili iliyopita wamepoteza Mechi 3 tu wakiwa kwao.
 
##LA LIGA Ratiba##
 
Ijumaa Februari 3
2245 Deportivo La Coruna v Real Betis
 
Jumamosi Februari 4
1500 Malaga CF v RCD Espanyol
1815 FC Barcelona v Athletic de Bilbao
2030 Atletico de Madrid v CD Leganes
2245 Valencia C.F v SD Eibar
 
Jumapili Februari 5
1400 Sevilla FC v Villarreal CF
1815 Sporting Gijon v Deportivo Alaves
2030 Real Sociedad v Osasuna
2245 Celta de Vigo  v Real Madrid CF
 
Jumatatu Februari 6
2245 Granada CF v Las Palmas
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment