KIUNGO
Yaya Toure amerejeshwa Kikosini mwa Manchester City kwa ajili ya Mechi
zao za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL.
Toure,
mwenye Miaka 33, hakusajiliwa kwa ajili ya Mechi za Makundi za UCL na
pia kutupwa nje ya Kikosi cha Kwanza cha Man City baada ya Meneja wa
Timu hiyo Pep Guardiola kuingia kwenye Bifu na Wakala wa Gwiji huyo
kutoka Ivory Coast.
Wakala Dimitri Seluk alimjia juu Guardiola na Meneja huyo kuapa Toure hatakuwemo Kikosini mwake hadi aombwe radhi.
Wakala
huyo hakuomba radhi na ikabidi Yaya Toure mwenyewe achukue jukumu hilo
na kuanzia Novemba, Kiungo huyo akarejeshwa Kikosi cha Kwanza.
Kwenye UCL, Toure anachukuwa Nafasi ya Ilkay Gundogan ambae ni Majeruhi.
Man City wataivaa AS Monaco hapo Februari 21 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL.
UEFA CHAMPIONZ LIGI RATIBA
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku Saa za Bongo**
Jumanne 14 Februari 2017
Benfica v Borussia Dortmund
Paris Saint Germain v Barcelona
Jumatano 15 Februari 2017
Bayern Munich v Arsenal
Real Madrid v Napoli
Jumanne 21 Februari 2017
Bayer 04 Leverkusen v Atlético Madrid
Manchester City v Monaco
Jumatano 22 Februari 2017
FC Porto v Juventus
Sevilla v Leicester City
Jumanne 7 Machi 2017
Arsenal v Bayern Munich
Napoli v Real Madrid
Jumatano 8 Machi 2017
Barcelona v Paris Saint Germain
Borussia Dortmund v Benfica
Jumanne 14 Machi 2017
Juventus v FC Porto
Leicester City v Sevilla
Jumatano 15 Machi 2017
Atlético Madrid v Bayer 04 Leverkusen
Monaco v Manchester City
0 Maoni:
Post a Comment