Muda
ukiwa unahesabika kuelekea mchezo wao dhidi ya Simba, Kocha Mkuu wa
Majimaji, Muingereza, Kally Ongala amesema haoni sababu ya kushindwa
kuifunga Simba kwa kuwa wapo katika hatari ya kushuka daraja.
Simba
ambayo inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 45 nyuma ya vinara wa
ligi hiyo Yanga wanaoongoza kwa pointi 46, Jumapili hii inatarajia
kucheza na Majimaji mkoani Songea kwenye Uwanja wa Majimaji ambapo kwa
sasa wapinzani wao hao wanakamata nafasi ya 14 wakiwa na pointi 20.
Akizungumza
Ongalla alisema kutokana na kutopata muda mrefu wa kufanya maandalizi
yao hawana sababu yoyote ya kushindwa kuifunga Simba kwa kuwa wapo
kwenye wakati mgumu.
"Kiukweli
tunashukuru tunaendelea na maandalizi kwa kuwa muda umekuwa wa kutosha
hivyo tutahakikisha tunaifunga Simba kwa sababu hatupo katika nafasi
nzuri hivyo ushindi kwetu ni kitu muhimu.
“Unajua
Simba ni timu nzuri kwa sababu hata ukiangalia wapo katika nafasi nzuri
kwenye msimamo tofauti na sisi, sasa hilo hatutaki kulipa nafasi kwa
kuwa tunachokiangalia ni suala la matokeo hivyo wao wajue kuwa lazima
huku watuachie pointi tatu," alisema Ongalla.
0 Maoni:
Post a Comment