MAN UNITED YAIPIKU BARCA KWA 'UBORA' ULAYA!


Picha inayohusiana

MOURINHO ALALAMA 'KUBAGULIWA'!
WAKATI Timu yake Manchester United ikiipiku Barcelona kwa 'Ubora' huko Ulaya kwa mwendelezo wa kutofungwa katika Mechi nyingi za Ligi, Meneja wa Jose Mourinho amelalama kuhusu Marefa kumchukulia yeye tofauti.
 
Jana kwenye EPL, Ligi Kuu England, Man United ilitoka 0-0 na Hull City na hiyo ilikuwa Mechi yao ya 14 bila kufungwa kwenye Ligi.
 
Mara ya mwisho kwa Man United kuonja kichapo ni Oktoba walipofungwa na Vinara wa EPL Chelsea huko Stamford Bridge.
 
Wimbi hilo limeifanya Man United kuwa kileleni kwenye Ligi 5 kubwa Barani Ulaya kwa kuongoza kwa kutofungwa katika Ligi kwa muda mrefu kupita Timu yeyote.
 
Waliokuwa wakishika hatamu ni Mabingwa wa Spain Barcelona ambao hadi sasa hawajafungwa katika Mechi 13.
 
Katika Listi hiyo ya Timu za juu Ulaya ambazo hazijafungwa muda mrefu pia wamo Tottenham ambao wana Mechi 8 za EPL bila kufungwa.
 
Kwa Ulaya, Timu inayoshikilia Nafasi ya 3 ni Napoli ambayo haijafungwa Mechi 11 za Serie A.
 
Wakati huo huo, Meneja wa Man United Jose Mourinho amelalamika na kudai yeye anaamuliwa kwa Sheria tofauti ukilinganisha na Mameneja wengine wa EPL.
 
Jana, kwenye Mechi na Hull City, Mourinho alichukizwa na Refa Mike Jones kwa kushindwa kuwadhibiti Hull waliokuwa wakipoteza muda mno ili kulinda Sare yao na Mreno huyo kuongea na Refa wa Akiba.
Tokeo la picha la MOUNRIHO
Mourinho ameeleza: "Mnajua wazi mie niko tofauti. Sheria kwangu zipo tofauti."
 
Aliongeza: "Jana Refa wa Akiba alimwambia Meneja: 'Nafurahia sana msisimko wako'. Leo mie naambiwa kaa chini au tutakutoa Uwanjani!"
 
Msimu huu tayari Mourinho ameshatwangwa Vifungo Viwili kutokana na kuongea kuhusu Refa na pia kupiga Teke Chupa ya Maji akiwa Uwanjani.
 
Share on Google Plus

About KASSIM OMARY

HII NI BLOG AMBAYO ITAKUWA INAKUPA HABARI MOTOMOTO ZA KIMICHEZO NA HABARI KWA UJUMLA
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment