Chelsea wako kifua mbele katika
ligi na alama 9 na wanaweza kujiimarisha kileleni wakati wakiipokea
Arsenal ilio nafasi ya tatu.
Mechi hii kwa Chelsea ni fursa
kujivua aibu baada ya kulambishwa sakafu na arsenal bao tatu kwa bila
katika mechi ya awali.
Na baada ya hapo ndio ulikuwa mwanzo mzuri wa Chelsea kufululiza na matokeo mazuri .
Arsenal ambao jumanne walipokea kichapao cha Watford , wana wasiwasi
mkubwa hasa baada ya kiungo wake Aron Ramsey kuumia mguu.
Pia
watakosa huduma za Granit Xaka anayetumikia adhabu huku Mohamed
Elneny akiwa michezo ya fainali za kombe la Afrika na timu yake ya
Misri.
Ushindani pia ni kati ya washambuliaji wawili Diego Costa
wa Chelsea na Alexis Sanchez ambao wanaongoza kama wafungaji bora na
mabao 15.
Katika mechi nyingine hapo kesho Tottenham ilio nafasi ya pili wanaipokea Middlesbourg.
Nayo Liverpool itasaka ushindi wake wa kwanza mwaka huu wakiwa ni wageni wa Hull City.
Jumapili, Manchester City wanachuana na Swansea City huku Leicester City wakiikaribisha Man U.
0 Maoni:
Post a Comment