Mshindi
wa nishani ya dhahabu mwaka 2012 katika mbio za mita 800 za huko London
Mariya Savinova, amevulia taji lake na kupigwa marufuku kushiriki
mashindano yoyote ya mbio hadi mwaka 2019.
Matokeo yote ya mbio za
mwanariadha huyo tangu Julai 10, 2010 hadi Agosti 2013, zimefutiliwa
mbali, baada ya kupatikana ametumia dawa za kusisimua misuli.
Savinova
alimpiku Caster Semenya wa Afrika Kusini katika mashindano hayo ya
Olimpiki Jijini London na pia mbio za dunia za riadha mwaka 2011 huko
Daegu, Korea Kusini.
Mkimbiaji huyo mwenye umri wa miaka 31 pia
alimshinda Muingereza Jenny Meadows katika mbio za mataifa ya Bara Ulaya
mwaka 2010 na kumfanya kunyakua medali ya shaba.
Sasa medali zote za
wanariadha hao wawili Jenny Meadows na Caster Semenya zitaboreshwa.
Savinova
pia atapoteza dhahabu yake katika mbio za mita 800 ya mwaka 2011 pale
aliposhinda mashindano ya mataifa bingwa barani Ulaya.
Taarifa
kutoka katika mahakama inayosikiliza makosa ya kimichezo: "Kwa misingi ya
ushahidi tosha, ikijumuisha pia ushahidi kutoka kwa hati ya kuzaliwa
(ABP), Mariya Savinova amepatikana akijihusisha na utumiaji wa dawa za
kusisimua misuli tangu Julai 26, 2010 (Usiku wa kuamkia mashindano ya
mataifa bingwa Ulaya yaliyokuwa yakifanyikia mji wa Barcelona) muda
wote hadi Agosti 19, 2013 (siku ya mashindano ya dunia Jijini Moscow).
Savinova
ni miongoni mwa wanariadha watano wa Urusi waliotajwa katika ripoti ya mamlaka kuu ya kukabiliana na dawa za kusisimua misuli miongoni mwa
wanariadha (WADA).
Hajashiriki mbio tangu mwaka 2013 pale
aliposimamishwa ili achunguzwe baada ya video kuhusu matumizi ya madawa
hayo kufichuliwa na mpekuzi Yuliya Stepanova.
0 Maoni:
Post a Comment