Mwanariadha wa Kenya Peres Jepchirchir ameweka rekodi mpya ya dunia katika mbio za half marathon.
Jepchirchir
alimaliza mbio hizo kwa muda was aa moja, dakika tano na sekunde sita
katika mbio za half marathon za Ras al-Khaimah katika Umoja wa Milki za
Kiarabu.
Muda wake ulikuwa sekunde tatu bora ukilinganisha na
rekodi ya awali iliyowekwa na Mkenya mwingine Florence Kiplagat mjini
Barcelona miaka miwili iliyopita.
Rekodi hiyo hata hivyo bado itahitaji kuthibitishwa na shirikisho la riadha duniani, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.
0 Maoni:
Post a Comment