FIFA imefafanua ni kwa namna gani timu 48 zitaweza kushiriki michuano hiyo.
Rais
wa shirikisho la soka Ulaya Aleksander Ceferin amesema kuwa
amefurahishwa na hatua hiyo na nchi za Ulaya zitawakilishwa vyema.
Mchakato huo utakuwaje?
Kila mwanachama wa FIFA atakuwa na uwezo wa kuongeza walau timu moja katika michuano ya mwaka 2026.
Mwenyeji wa fainali hizi ataingia moja kwa moja kama ilivyokua awali.
Mapendekezo hayo yapo hivi
Afrika - 9 kutoka timu za awali 5
Asia - 8 kutoka timu 4 za awali
Ulaya - 16 kutoka timu 13 za awali
Marekani ya Kaskazini, Kati na Caribbean - 6 kutoka timu 4 za awali
Bara la Oceania - 1 kutoka timu 1 ya awali
Amerika ya Kaskazini - 6 kutoka timu 4 za awali
Mwezi januari chama hicho chenye mamlaka makubwa ya
soka duniani, kilipanga kuongeza timu zitakazoshiriki michuano ya kombe
la dunia kutoka 32 mpaka 48 na hii itaanza mwaka 2026.
0 Maoni:
Post a Comment