LICHA
ya wachezaji wa Yanga kutolipwa mishahara ya miezi mitatu, lakini
wamepanga kuingia uwanjani kwa nia moja tu pekee ya kuwafunga wapinzani
wao Zanaco ya Zambia huku viongozi wao wakishughulikia tatizo hilo.
Timu
hizo, zinatarajiwa kujitupa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
leo katika mechi ya hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mshindi
wa mechi ya leo atafuzu hatua ya makundi na atakayefungwa atashushwa
kucheza Kombe la Shirikisho Afrika akicheza mechi mbili za mtoano na
timu za huko kuwania kufuzu Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho.
Chanzo kimeleza viongozi wa timu hiyo wanashughulikia mishahara hiyo na wakati wowote wanatarajiwa kulipwa.
Wachezaji
hao walifanya kikao cha wao wenyewe mara baada ya kumalizika kwa
mazoezi ya mwisho ya timu hiyo yaliyofanyika jana asubuhi kwenye Uwanja
wa Taifa.
Katika
kikao hicho, wachezaji walionekana kupeana mioyo ya kijasiri huku
wakiweka matatizo yao pembeni na badala yake kuhamasishana ili washinde
kwenye mechi ya leo kabla ya kurudiana Lusaka, Zambia.
“Wachezaji
wote tunatakiwa kuungana na tuwe kitu kimoja ili kuipambania timu yetu
kwa lengo la kupata mtaji mkubwa wa ushindi kabla ya kurudiana nyumbani
kwao.
“Ninaamini
kuwa, kama tukishinda mechi hii viongozi watahamasika na kushawishika
kutulipa mishahara yetu ya miezi mitatu, hivyo kila mchezaji atakayepata
nafasi ya kucheza, basi anatakiwa kupambana ili tushinde mchezo huu,”
alisikika mmoja wa wachezaji akizungumza hayo.
0 Maoni:
Post a Comment