Arsene Wenger, ameihudumia kama meneja
wa klabu ya Arsenal kwa miaka 21 lakini wiki hii imeweka hatma yake ya
miaka ijayo katika wasiwasi kuliko wakati mwengine ule wowote katika
uongozi wake.
Kubanduliwa kwa mara ya saba katika hatua ya kumi
na sita bora katika ligi ya kombe la vilabu bingwa Ulaya ulikuwa
uchungu wa kutosha, bila kuongeza pigo la magoli 10-2 kutoka kwa
Bayern Munich.
Malalamiko dhidi ya Wenger yamekuwa yakisikika chini kwa chini kwa miaka mingi lakini sasa malalamiko hayo yameongezeka .
Kwa
mwaka huu wote, mkataba mpya bado uko mezani, huku meneja huyo mwenye
umri wa miaka 67 akisema maoni ya mashabiki yatachochea uamuzi wake
iwapo atasalia kama meneja.
Wenger kila mara hukosolewa na vyombo vya habari, na mashabiki wengi wamezoea kupata habari na mabadiliko na sio uthabiti wake.
Alisema maneno sawa na hayo yeye mwenyewe .
Liverpool
hawajawahi shinda ligi ya Uingereza na Manchester United wamechukua
muda tangu kushiriki katika ligi ya Vilabu bingwa Ulaya lakini wawili
hao wamekuwa na zaidi ya mameneja mmoja ndipo hawakosolewi mara
nyingi.
0 Maoni:
Post a Comment