Kiungo mwenye kasi wa Mbeya City, Mrisho Ngassa, amefunguka kuwa yupo
mbioni kuachana na klabu yake ya sasa ya Mbeya City mara baada ya
kumalizika mkataba wake mwishoni mwa msimu huu.
Ngassa alijiunga na Mbeya City katika usajili wa dirisha dogo msimu huu
akitokea Fanja FC ya Oman, amesema mkataba ukiisha amepanga kuondoka
kwenda Oman.
“Mkataba niliosaini hapa (Mbeya City) ni wa muda mfupi, hivyo sitarajii
kuongeza mwingine. Niliondoka Fanja kwa sababu kibali changu kilikuwa na
matatizo na ndiyo maana nilirudi hapa Bongo, lakini mipango yangu
ikikaa sawa nitarejea kule,” alisema Ngassa.
Ngassa alijiunga na Fanja akitokea Free State Star ya Afrika Kusini ambayo alivunja nayo mkataba na kwenda Oman.
Lakini kabla, akiwa hapa nchini Ngassa alianza kuonyesha cheche akiwa na
Toto Africans ya kwao Mwanza kabla ya kujiunga na Kagera Sugar na
kuonyesha uwezo mkubwa na kuivutia Yanga.
Timu nyingine kubwa alizozichezea baada ya Yanga ni Simba ambayo alijiunga nayo akitokea Azam FC.
0 Maoni:
Post a Comment