Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino amedokeza kwamba "haiwezekani" kwake kuwa meneja wa klabu ya Barcelona ya Uhispania.
Mkufunzi
huyo wa zamani wa klabu ya Espanyol alikutana na rais wa Barca Josep
Maria Bartomeu wiki iliyopita huku uvumi ukiongezeka kwamba huenda
akamrithi Luis Enrique.
Hata hivyo, BBC imefahamu kwamba yeye si miongoni mwa wanaotathminiwa kwa ajili ya kupewa kazi hiyo.
"Mimi
ni shabiki wa Espanyol - Nafikiri sihitaji kusema sana kuhusu hilo,"
raia huyo wa Argentina alisema, akisisitiza uhasama kati ya Espanyol na
majirani zao wa jiji Barcelona.
Pochettino, 45, pia alichezea Espanyol mechi 216.
Katika
kikao na wanahabari Alhamisi Pochettino alisema:
"Ni kama siku moja,
iwapo (mwenyekiti wa Spurs) Daniel Levy atanifuta kazi, haiwezekani
kwangu kuwa mkufunzi wa BARCELONA."
Taarifa zinasema Spurs walifahamu kuhusu mkutano wa POchettino na rais huyo wa Barca.
Mkufunzi msaidizi wa Barca Juan Carlos Unzue anapigiwa upatu kumrithi Enrique ambaye anaondoka mwisho wa msimu.
Mkufunzi wa Athletic Bilbao Ernesto Valverde pia anaaminika kuwa miongoni mwa wale ambao wanaweza kupewa kazi hiyo.
0 Maoni:
Post a Comment